• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ununuzi wa umeme wa Kenya kutoka Uganda wafikia mara tatu

    (GMT+08:00) 2017-11-17 18:51:16
    Kenya imeendelea kuongeza uagiziaji wa umeme kutoka nchi jirani ya Uganda ikiwa sasa kiwango hicho kimeongezeka mara tatu ndani ya miezi nane ya kwanza ya 2017.

    Hadi sasa taakwimu zinaonyesha kuwa Kenya imeagiza umeme wa thamani ya dola milioni 33.7.

    Kilowati moja ya umeme kutoka Uganda ni shilingi 21 kulingana na makubaliano yaliotiwa saini kati ya nchi hizo mbili mwaka 2014.

    Tume ya kuthibiti kawi nchini Kenya imesema umeme unaonunuliwa Uganda hasa unatumika katika maeneo ya Maghribi baada ya ukame kuathiri bwawa la kuzalisha kawi ys Sondu Miriu.

    Lakiniu hata hivyo shilingi 21 kwa kilowati moja ni mara 7 ya bei ya umeme unaozalisha ndani ya nchi nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako