• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yawakamata wapiganaji 19 wa kundi la Al Shabaab katika operesheni ya kijeshi

    (GMT+08:00) 2017-11-17 18:53:14

    Serikali ya Somalia imesema kuwa imewakamata wapiganaji 19 wa kundi la Al Shabaab katika mkoa wa kusini wa Lower Shabelle.

    Waziri wa Habari wa Somalia Abdirahman Omar Osman amesema, watuhumiwa hao, akiwemo mtaalam wa vifaa vya mlipuko, walikamatwa katika eneo la Afgooye, kilomita 30 magharibi mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.

    Kukamatwa kwa wapiganaji hao kumetokea siku moja baada ya serikali kutangaza majina na picha za watu sita ambao inasemekana kuwa walihusika na shambulizi la kigaidi la Oktoba 14 mjini Mogadishu ambapo watu zaidi ya 350 waliuawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako