• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Morocco wazungumza

    (GMT+08:00) 2017-11-17 19:07:23

    Waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Wang Yi leo hapa Beijing amefanya mazungumzo na mwenzake wa Morocco Nasser Bourita, ambapo wamesaini kumbukumbu ya kushirikiana kuhimiza utekelezaji wa pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Bw. Wang amesema, China inapenda kushirikiana na Morocco kupanua zaidi ushirikiano halisi katika sekta mbalimbali, kuimarisha uratibu katika masuala makubwa ya kimataifa na ya kikanda, na kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea.

    Bw. Nasser Bourita amesema, China ni mwenzi wa kutegemeka na kuaminika wa Morocco, na anatumai kuwa Morocco itashirikiana na China katika mambo ya kisiasa, kupambana na ugaidi na masuala makubwa ya kimataifa. Pia amesema nchi hizo zitapanua zaidi ushirikiano wa kunufaishana katika uwekezaji na biashara, na ujenzi wa reli, na kukaribisha kampuni za China kukuza soko la Afrika na la nchi za Kiarabu kwa kutumia nafasi ya jiografia ya Morocco.

    Mjumbe wa taifa wa China Bw. Yang Jiechi leo pia amekutana na Bw. Bourita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako