• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya mambo ya nje ya Zimbabwe na jeshi la ulinzi wa taifa zakanusha kutokea kwa uasi

    (GMT+08:00) 2017-11-17 19:09:56

    Maofisa kutoka wizara ya mambo ya nje ya Zimbabwe na jeshi la ulinzi la nchi hiyo wamekutana na waandishi wa habari na kukanusha kutokea kwa uasi nchini humo.

    Katika mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na mabalozi na wawakilishi wa nchi mbalimbali nchini Zimbabwe, Jeshi hilo limesema rais Robert Mugabe wa nchi hiyo yuko salama, na wananchi wa Zimbabwe na raia wa kigeni wanaoishi nchini Zimbabwe hawana haja ya kuwa na wasiwasi na usalama wao.

    Katibu wa wizara ya mambo ya nje ya Zimbabwe Bw. Joey Bimha amesema, jumatano alfajiri jeshi lilichukua hatua ya kudhibiti wizara muhimu za serikali, na kuwakamata wahalifu walioharibu maendeleo ya uchumi na jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako