• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan na Marekani kuendelea na mazungumzo kurejesha uhusiano wa kawaida kati yao

    (GMT+08:00) 2017-11-17 19:11:42

    Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Ibrahim Ghandour amekutana na kufanya mazungumzo na naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Sullivan mjini Khartoum kwa lengo la kurejesha uhusiano wa kawaida kati ya nchi hizo.

    Bw. Ghandour amesema, kitendo cha Marekani kuondoa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Sudan ni muhimu sana kwa kurejesha uhusiano wa kawaida kati ya nchi hizo mbili.

    Kwa upande wake, Bw. Sullivan amesema, Marekani na Sudan zitaanzisha mchakato mpya wa kuongeza uhusiano wa pande mbili na kuendelea kudumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo ya uhusiano kati yao.

    Nchi hizo mbili pia zimejadiliana kuhusu ushirikiano wa sekta kadhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako