• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Mashariki imetolewa wito wa kufungua anga ili kurahisisha usafiri wa ndege

    (GMT+08:00) 2017-11-18 16:59:35

    Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga IATA limehimiza ukanda wa Afrika Mashariki kufungua maeneo yake ya anga ili kuwawezesha wasafiri na waendeshaji kusafiri kwa urahisi katika ukanda huo.

    Naibu mwenyekiti wa IATA kwa Afrika Raphael Kuuchi amesema imetimia karibu miaka 20 tangu nchi za ukanda huo kusaini Makubaliano ya Yamoussoukro mwaka 1999, lakini kushindwa kuyatekeleza kumekwamisha maendeleo ya usafiri wa anga wa ukanda huo na gharama ya usafiri ya ndege kuwa juu.

    Kuuchi ameliambia shirika la habari la China Xinhua kuwa serikali za nchi za Afrika Mashariki zinatakiwa kukubali kufungua maeneo yao ya anga ili kupunguza gharama na kuongeza uwezo wa kusafiri kwa ndege, na pia kukubali kuwa safari za ndege katika ukanda huo ni za ndani, ama sivyo hakuna njia nyingine ya kuongeza safari za ndani au za kikanda.

    Wakati huohuo, shirika la ndege la Kenya limesema litazingatia soko la Afrika ili kuongeza mapato yake. Hivi sasa maeneo 40 kati ya 53 inayoyahudumia Shirika hilo yapo barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako