• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wito wa kumtaka Mugabe ajiuzulu waongezeka ndani ya chama tawala nchini Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2017-11-18 17:00:21

    Kamati nane kati ya kumi za ngazi za mikoa za Chama tawala cha ZANU-PF nchini Zimbabwe zimetoa wito kwa rais Robert Mugabe kuondoka madarakani.

    Wito huo ulitolewa baada ya jeshi kudhibiti serikali mapema wiki hii.

    Mikoa hiyo ukiwemo mkoa alikozaliwa wa Mashonaland West imemtuhumu Mugabe kwa kuruhusu kuundwa kwa makundi ya njama na kumtaka Mugabe atangaze kuvunja uhusiano wake na kundi la G40 linalotuhumiwa kuongozwa na mkewe Grace Mugabe.

    Wakati huohuo, mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC Jacob Zuma amesema jumuiya hiyo iko tayari kutoa misaada yote inayohitajika kusaidia watu wa Zimbabwe kushughulikia msukosuko wa kisiasa wa sasa, na haitaki kuona mabadiliko ya madaraka kinyume cha sheria yatokee nchini Zimbabwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako