• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lashindwa kupitisha azimio kuhusu uchunguzi wa mashambulizi ya kikamikali nchini Syria

    (GMT+08:00) 2017-11-18 17:00:49

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kupitisha azimio lililoandaliwa na Japan la kuongeza muda wa siku 30 kwa utaratibu wa uchunguzi wa pamoja wa mashambulizi ya kikamikali nchini Syria, ambao umemalizika Ijumaa.

    Azimio hilo lilipigiwa kura za ndiyo 12, za hapana 2 na kura moja iliharibika. Russia ikiwa nchi mjumbe wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ilitumia kura ya veto dhidi ya azimio hilo, na China haikupiga kura.

    Naibu balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa Wu Haitao amesema hatua ya Baraza la Usalama inapaswa kuangalia mchakato wa jumla wa kisiasa nchini Syria. Ameongeza kuwa pande mbalimbali zinatakiwa kujidhibiti na kutafuta ufumbuzi unaoridhisha pande zote kupitia mazungumzo yenye uvumilivu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako