• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Panama inapenda kushiriki katika ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

    (GMT+08:00) 2017-11-19 17:03:54

    Rais Juan Carlos Varela wa Panama amesema nchi yake inaunga mkono ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na kupenda kuunganisha mikakati ya maendeleo ya Panama na pendekezo hilo.

    Rais Varela ambaye yuko ziarani nchini China pia amesema Panama itatumia nafasi yake ya kijiografia kuhimiza nchi nyingine za Latin Amerika kushiriki kwenye pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na pia taasisi za kifedha nchini Panama zinafanya utafiti kuhusu miradi itakayoweza kuorodheshwa katika pendekezo hilo.

    Amekumbusha kuwa alipofanya ziara kwa mara ya kwanza nchini China mwaka 2007, alishangazwa na kuonea wivu maendeleo ya kiuchumi ya China, na kuanzia hapo amekuwa na fikra imara ya kufuata sera ya kuwepo kwa China moja na kukuza urafiki na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako