• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa dola za kimarekani milioni 6 kusaidia Jamhuri ya Kongo

    (GMT+08:00) 2017-11-19 17:04:28

    Serikali ya China imetoa msaada wa dharura wa kibinadamu wa dola za kimarekani milioni 6 kwa Jamhuri ya Kongo ili kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na mgogoro wa kibinadamu uliosababishwa na machafuko yaliyotokea mkoani Pool, nchini humo.

    Waziri wa masuala ya kijamii na kibinadamu wa Jamhuri ya Kongo Antoinette Dinga Djondo ameishukuru serikali ya China baada ya ubalozi wa China nchini humo kutoa tangazo hilo. Amesema hadi sasa serikali ya Jamhuri ya Kongo imepata msaada wa dola za kimarekani milioni 12 baada ya kutoa ombi kwa jamii ya kimataifa, na nusu kati ya fedha hizo zimetolewa na China.

    Shirika la Mpango wa Chakula Duniani limesema, fedha za msaada zilizotolewa na serikali ya China ni nyingi zaidi zilizopokelewa tangu mpango wa msaada wa dharura uzinduliwe, na zitasaidia kutimiza lengo la utoaji msaada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako