• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya watu 12 wafariki kwenye ajali ya barabarani Magharibi mwa Kenya

    (GMT+08:00) 2017-11-19 17:48:38

    Kamanda wa polisi wa kaunti ya Nakuru, magharibi mwa Kenya Bw. Hassan Barua amesema, zaidi ya watu 12 wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa vibaya kwenye ajali ya barabarani iliyotokea mapema leo.

    Bw. Barua amesema, saa tisa alfajiri kwa saa za Kenya, basi moja lililokuwa na abiria 11 liligongana na lori moja kwenye barabara ya Nakuru –Eldoret. Dereva wa basi na abiria 11 wote wamefariki, na dereva wa lori na abiria mmoja wa lori wamejeruhiwa vibaya,

    Kamanda huyo amesema, ajali nyingi za barabarani zimetokea katika eneo hatari la Salgaa na kusababisha vifo vya wasafiri wengi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako