• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hali ya Gaza inaendelea kuwa ngumu kutokana na vizuizi

    (GMT+08:00) 2017-11-20 09:24:10

    Msemaji wa shirika la misaada na kazi la Umoja wa Mataifa kwa wakimbizi wa Palestina UNRWA Bw. Christopher Gunness, ametahadharisha kuhusu hali ngumu kwa shirika hilo na ukanda wa Gaza, kutokana na kizuizi kilichowekwa dhidi ya Gaza.

    UNRWA inakabiliana na hali ngumu kifedha huku msukosuko wa kibinadamu ukiongezeka katika sehemu hiyo, hali inayowafanya wakimbizi wa Palestina waendelee kutegemea zaidi msaada wa huduma za UNRWA.

    Bw. Gunness amesema kwa sasa kuna upungufu wa dola za kimarekani milioni 77 kwenye bajeti ya shirika hilo, ambao ni mkubwa na usiokubalika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako