• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia, Iran na Uturuki zaandaa mazungumzo ya kitaifa ya Syria

    (GMT+08:00) 2017-11-20 09:55:32

    Mawaziri wa mambo ya nje wa Russia, Iran na Uturuki wamekutana mjini Antalya, Uturuki kujadili maandalizi ya mazungumzo ya kitaifa ya Syria, yanayotarajiwa kufanyika mjini Sochi, Russia.

    Wizara ya mambo ya nje ya Russia imetoa ripoti ikisema, mkutano huo una lengo la kurejesha uaminifu kati ya pande mbalimbali za Syria, na kutafuta suluhisho na kufikia makubaliano yatakayosaidia kujenga Syria yenye umoja na nguvu.

    Mawaziri hao wamesema kiwango cha matumizi ya mabavu nchini Syria kimepungua, hali inayotoa nafasi kwa pande zilizopambana nchini Syria zitafute ufumbuzi wa kisiasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako