• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msomi wa Kenya asema, ustaarabu wa kiikolojia wa China ni muhimu kwa utulivu wa dunia

    (GMT+08:00) 2017-11-20 09:55:53

    Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya sera za Afrika nchini Kenya Bw. Peter Kagwanja amesema, ustaarabu wa kiikolojia wa China utasaidia kutuliza utaratibu wa dunia, ambao umeathiriwa na ongezeko la idadi ya watu, mabadiliko ya hali ya hewa, migogoro, kudorora kwa uchumi na ugaidi.

    Bw. Kagwanja amesema, ustaarabu wa kiikolojia wa China umethibitishwa kuweza kuzuia athari za kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiikolojia kwa ulimwengu wa kisasa, na kwamba katika miaka ya hivi karibuni, China imetambua ustaarabu wa kiikolojia kama sehemu ya juhudi za kukabiliana na hali zisizotabirika kwenye utaratibu wa kimataifa ulioathiriwa.

    Amesema hivi sasa, China imekuwa mfano wa kuigwa kwa nchi nyingine zinazoendelea, kwa kuunganisha vizuri mageuzi ya soko na mambo ya kidemokrasia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako