• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe asema ataitisha mkutano mkuu wa chama mwezi ujao

    (GMT+08:00) 2017-11-20 09:57:39

    Rais Robert Mugabe wa Ziimbabwe alipohutubia taifa jana usiku kupitia televisheni, alisema ataitisha mkutano mkuu wa chama cha ZANU-PF mwezi Desemba ili kutatua masuala yanayokikabili chama hicho.

    Hotuba hiyo imetolewa baada ya chama cha ZANU-PF kumtaka ajiuzulu nyadhifa zake za kiongozi wa chama na rais wa nchi.

    Rais Mugabe amesema mapambano ndani ya chama yataharibu uchumi wa Zimbabwe unaokabiliwa na hali ngumu, pia yatavunja mshikamano wa taifa. Ametaja kuwa mapambano hayo yamesababishwa na pengo kati ya vizazi viwili, ambapo wanachama wakongwe wanatakiwa kukubali kanuni mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako