• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa nchi za kiarabu walaani Iran kuingilia mambo ya nchi za kiarabu

    (GMT+08:00) 2017-11-20 09:58:07

    Mawaaziri wa mambo ya nje wa nchi za kiarabu wameilaani Iran kwa kuingilia kwenye mambo ya nchi za kiarabu, na wameliomba kundi la nchi za kiarabu kwenye Umoja wa Mataifa limfahamishe mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu uingiliaji wa Iran.

    Katika taarifa iliyotolewa baada ya mkutano maalumu ulioitishwa na Saudi Arabia, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za kiarubu wamesema watawasilisha ombi kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzu kuhusu Iran kukiuka Azimio nambari 2231, kwa mpango wake wa kuendeleza makombora.

    Mawaziri hao pia wamesema Iran imeipatia Yemen kombora lililotumiwa kuishambulia Saudi Arabia, inayapatia silaha makundi ya kigaidi nchini Bahrain, yanayopewa silaha na mafunzo na kundi la Hezbollah la Lebanon na jeshi la Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako