• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Joseph Areruya aibuka bingwa mbio za baiskeli Rwanda

    (GMT+08:00) 2017-11-20 10:08:57
    Joseph Areruya wa Rwanda ndiye bingwa mpya wa mashindano ya kimataifa ya Baiskeli (Tour du Rwanda) yaliyomalizika jana mjini Kigali.

    Nyota huyo amibuka mshindi wa jumla kwa kutumia saa 20 kakika 21 na sekunde 29 katika mbio hizo zenye umbali wa kilomita 819.

    Katika mbio hizo zilizojumuisha nyota 83 kutoka mataifa mbalimbali, waendesha baiskeli watatu kutoka Rwanda wamefanikiwa kuingia tano bora ambao ni Joseph Areruya, Jean Bosco Nsengimana na Patrick Byukusenge.

    Licha ya kushinda katika hatua ya mwisho ya mbio hizo yenye umbali wa kilomita 120, Bingwa wa mwaka 2016 Valens Ndayisenga hakuweza kutetea na aliishia nafasi ya sita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako