• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalam wasema mafanikio ya China ni muhimu kwa nchi za Afrika

    (GMT+08:00) 2017-11-20 18:01:22

    Wataalam wamesema China imepata mafanikio makubwa chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na uzoefu wake ni muhimu kwa maendeleo ya Rwanda na nchi nyingine za Afrika.

    Akizungumza na Shirika la Habari la China Xinhua, mjumbe wa Kamati Kuu ya chama tawala cha Rwanda RPF Abdul Karim Harelimana amesema China imekuwa na utulivu wa kisiasa na msingi imara wa kiuchumi, hivyo CPC iko kwenye mwelekeo sahihi na chama hicho kimeweza kutimiza matokeo chanya yanayoonekana dhahiri katika miaka mitano iliyopita nchini China.

    Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utawala ya Rwanda Anastase Shyaka amesema, mafanikio ya China yametokana na uongozi imara unaofanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya nchi nzima na si kwa maslahi binafsi.

    Katika miaka 30 iliyopita, China imefanikiwa kuwaondoa watu milioni 700 kutoka kwenye umasikini uliokithiri, hivyo kupiga hatua kubwa kwenye kazi ya kupunguza umasikini duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako