• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SADC kujadili suala la Zimbabwe huko Angola

    (GMT+08:00) 2017-11-20 18:11:13

    Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC itafanya mkutano huko Angola, ili kujadili kuhusu suala la Zimbabwe.

    Viongozi wa Afrika Kusini, Angola, Tanzania na Zambia kesho watakutana huko Angola. Mwenyekiti wa zamu wa jumuiya hiyo rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amemtuma balozi maalumu kwenda Zimbabwe kukutana na pande husika za nchi hiyo.

    Rais Zuma amesisitiza tena kuwa jumuiya hiyo inapinga mabadiliko ya mamlaka ya kisiasa yasiyofuata katiba, huku akisema, jumuiya yenye utulivu na amani inaendana na maslahi ya nchi wanachama, ambapo Zimbabwe ni moja ya nchi wanachama muhimu wa jumuiya hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako