• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Korea Kusini kufanya juhudi kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kwa njia sahihi na tulivu

    (GMT+08:00) 2017-11-20 18:16:46

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang hapa Beijing amesema, China inaitaka Korea Kusini kuendelea kufanya juhudi kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kwa njia yenye usahihi na utulivu, na kusema China siku zote inahimiza uhusiano kati yake na Korea Kusini katika msingi wa kuheshimiana na kunufaishana.

    Waziri wa mambo ya nje ya Korea Kusini Bw. Kang Kyung-Wha atafanya ziara nchini China kuanzia tarehe 21 hadi 23 mwezi huu. Akizungumzia ziara hiyo, Lu Kang amesema, ni muhimu kwa pande hizo mbili kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili kuhusu kuboresha na kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili, kuzidisha maelewano ya kisiasa, na kuheshimu maslahi muhimu na mambo yanayofuatiliwa na nchi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako