• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Magonjwa ya kudumu yamekuwa chanzo kikuu cha kifo cha raia wa China

    (GMT+08:00) 2017-11-20 19:05:31

    Shughuli ya kuadhimisha miaka 30 ya kamati ya kinga na tiba ya China ambayo pia ni mkutano wa tano wa kitaaluma wa mwaka imefanyika hapa Beijing. Hivi sasa magonjwa mbalimbali ya kudumu ukiwemo ugonjwa wa mishipa ya damu ya moyo na ubongo, ugonjwa wa kisukari na shinikizo la juu la damu yamekuwa chanzo kikuu cha vifo kwa raia wa China. Wataalamu wamesema, licha ya juhudi za idara za afya, umma unatakiwa kuinua kiwango cha afya na kuwa na tabia nzuri ya maisha, ili kupunguza kiwango cha kupata magonjwa ya kudumu.

    Mkuu wa kamati ya kinga na tiba ya China Bw. Wang Longde amesema, hivi sasa kiwango cha magonjwa ya kudumu kimeonesha mwelekeo wa kuongezeka, na kuwa tishio kubwa kwa afya kwa watu nchini China. Bw. Wang anasema,

    "Mambo yanayosababisha magonjwa ya kudumu, ukiwemo uzito kupita kiasi na unene yameongezeka kwa kiasi kikubwa, hivyo idadi ya wagonjwa pia imeongezeka kwa kasi. Kiwango cha vifo kinachosababishwa na magonjwa hayo kimeongezeka hadi kufikia zaidi ya asilimia 85, na kiwango cha vifo kinachotokana na magonjwa ya mishipa ya damu ya moyo na ubongo kimechukua zaidi ya asilimia 50".

    Magonjwa ya kudumu pia yanaitwa magonjwa yanayosababishwa na tabia na mtindo wa maisha. Mwanataaluma wa Taasisi ya Uhandisi ya China Bw. Liu Xu amesema, kufuatia kuboreshwa kwa hali ya maisha ya watu, hali ya lishe kwa umma pia imebadilika sana, na kuwa jambo muhimu linalosababisha magonjwa ya kudumu. Anasema,

    "Kutokana na hali ya lishe kwa umma, kalori wanazokula watu zimeanza kupungua, hali ya ulaji wa protini imekuwa tulivu. Lakini kiwango cha protini inayotokana na wanyama kimeongezeka kidhahiri, huku kiwango cha protini zinazotoka kwa mimea kikipungua. Ulaji wa mafuta umeongezeka kwa kiasi kikubwa, na kuwa chanzo kikuu cha magonjwa yanayotokana na virutubisho, ukiwemo unene. "

    Bw. Wang pia amehimiza kuboresha mkakati wa kinga na tiba, anasema,

    "Ili kuboresha mkakati wa kinga na tiba, lengo kuu la kazi ya afya ni nini? Lengo letu kuu ni kupunguza idadi ya wagonjwa kwa kiasi kikubwa, badala ya kutoa tiba kwa watu wanaopata magonjwa. Hii inamaanisha kuwa mkakati wetu umebadilika kutoka kiini cha tiba, na kuwa kutilia maanani afya ya umma. Kwa mujibu wa utafiti wa Shirika la Afya Duniani WHO, mtindo wa maisha na vitendo vinachukua asilimia 60 ya mambo yanayoathiri afya na maisha ya watu. Hivyo kurekebisha mtindo wa maisha na afya, kunaweza kukinga magonjwa mengi ya kudumu."

    Kutokana na mpango wa serikali ya China, hadi kufikia mwaka 2020 na 2025, kiwango cha vifo vinavyotokana na magonjwa ya kudumu, kinatarajiwa kupungua kwa asilimia 10 na 15 ikilinganishwa na mwaka 2015.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako