• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Serikali sasa kudhibiti mifugo ya nje

    (GMT+08:00) 2017-11-20 19:16:53

    Tanzania imetangaza kuchukua hatua za kudhibiti mifugo inayoingia nchini humo kinyume cha sheria na makubaliano ya kikanda na kimataifa.

    Katika taarifa iliyotolewa wiki hii , Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa vyombo vya habari ilibainisha kuwa, hatua zote zilizochukuliwa na serikali dhidi ya mifugo iliyokamatwa, zilifanyika kwa mujibu wa sheria na makubaliano hayo.

    Ilisema kumekuwepo taarifa katika baadhi ya vyombo vya habari na baadhi ya wanasiasa zinazoishutumu serikali kutokana na hatua ya kukamata na kupigamnada mifugo iliyoingizwa nchini bila kufuata sheria.

    Aidha, taarifa hiyo ilisema taarifa hizo zinajenga sintofahamu kuhusu suala la vifaranga vya kuku vilivyoteketezwa baada ya kuingizwa nchini bila kufuata sheria.

    Kuhusu suala la vifaranga, serikali ya Kenya ilimwita Balozi wetu aliyeko Nairobi kutaka maelezo na kutumia fursa hiyo kuelezea masuala haya kwa serikali ya Kenya.

    Ilitaja baadhi ya sheria hizo kuwa ni Sheria ya Magonjwa ya Wanyama Namba 17 ya Mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2007 na 2010, zinazotumika kudhibiti na kukagua uingizaji wa mifugo na mazao yake katika maeneo ya mpakani, bandarini na viwanja vya ndege.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako