• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Sekta ya sukari kuboreshwa Kenya

    (GMT+08:00) 2017-11-20 19:17:11

    Viongozi kutoka maeneo ya ukulima wa miwa wametoa wito wa utekelezaji wa mpango wa utoaji mazao ambapo wakulima wataumiliki mpango huo.

    Viongozi hao waliozungumza huko Kisumu wakati wa mkutano wa kitaifa wa wadau wa sekta ya sukari walitaka kubuniwa kwa idara chini ya wizara ya Kilimo itakayohusika na kusimamia kiwango cha sukari inayoagizwa kutoka nje.

    Swala hilo la uagizaji sukari kutoka nje ambalo wadau wanaamini limechangia mapato duni kwa wakulima lilijitokeza huku wajumbe wakitoa wito wa kusimamiwa kwa bidhaa hiyo kutoka nje ili kuhakikisha sukari inayoagizwa kutoka nje inakidhi mahitaji pekee .

    Magavana kutoka maeneo ya ukuzaji miwa walisema vitengo vilivyogatuliwa vina nafasi ya kuwatumia vyema wenye viwanda vya kusaga miwa kwa manufaa ya wakulima wa sehemu hizo.

    Gavana wa Kisumu Anyang Nyong'o alisema kwamba kubinafsishwa kwa viwanda vitano vinavyomilikiwa na serikali kunatarajiwa kuimarisha utendakazi na mashindano katika sekta ya sukari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako