• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michuano ya klabu bingwa Ulaya

    (GMT+08:00) 2017-11-21 09:14:11

    Usiku wa leo barani Ulaya nyasi za viwanja 8 katika miji tofauti zitawaka moto wakati mechi za raundi ya tano katika makundi E F G na G ya klabu bingwa zitakapopigwa.

    Katika Kundi E, Liverpool ya Uingereza itakuwa ugenini kucheza na Sevilla, zote zikiwa katika nafasi mbili za juu, huku Spartak Moscow ya Urusi ikicheza na NK Maribor ya Slovenia.

    Kundi F ni Manchester City dhidi ya Feyenoord ya Uholanzi, na Napoli watacheza na Shakthar Donetsk ya Ukraine.

    Na kundi katika kundi G, Besktas ya Uturuki itapambana na mabingwa wa mwaka 2004 FC Porto ya Ureno, na Monaco itakuwa na kibarua dhidi ya RB Leipzig ya Ujerumani.

    Apoel Nicossia watakuwa na kibarua kizito nyumbani nchini Cyprus kucheza na bingwa mtetezi wa michuano hiyo Real Madrid, na Borussia Dortmund itaikaribisha Tottenham ya Uingereza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako