• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watalii wa China wachangia dola za Marekani milioni 164 kwa Ethiopia katika mwaka 2016

    (GMT+08:00) 2017-11-21 09:20:24

    Ethiopia imeingiza pato la dola za Marekani milioni 164 kutokana na watalii wachina zaidi ya elfu 43 waliotembelea nchi hiyo mwaka jana.

    Mkurugenzi wa mahusiano ya umma na kimataifa wa wizara ya utamaduni na utalii Bw. Gezahegn Abate, amesema ukosefu wa vyakula na malazi ni kikwazo kwa ukuaji wa sekta ya utalii, licha ya kuwa idadi ya watalii kutoka China imeendelea kuongezeka katika miaka kadhaa iliyopita .

    Amesema wizara ya utamadamu inahimiza makampuni ya China kuwekeza kwenye sekta ya hoteli nchini humo ili kuvutia zaidi watalii wa China.

    Habari zinasema China imechukua nafasi ya tatu kwa idadi ya watalii wanaotembelea Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako