• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti yasema hadhi ya China inaongezeka katika minyororo ya thamani ya dunia

    (GMT+08:00) 2017-11-21 17:50:31

    Shirika la hakimiliki ya ubunifu la Dunia limetoa ripoti mpya ikionesha kuwa katika miaka ya hivi karibuni, hadhi ya China inaendelea kuongezeka katika minyororo ya thamani katika sekta ya utengenezaji ya dunia, na mashirika ya China yanaingia katika orodha ya mashirika yanayozalisha bidhaa zenye thamani ya nyongeza inayotokana na teknolojia ya juu.

    Kutokana na kutafiti shughuli za kahawa, betri inayozalisha umeme kwa nishati ya jua na simu za mkononi za kisasa, ripoti hiyo inayoitwa "Ripoti ya Hakimiliki ya Ubunifu ya Dunia 2017: mitaji isiyoonekana kwenye minyororo ya thamani ya dunia" imeonesha kuwa kwa bidhaa zinazouzwa kote duniani, karibu theluthi moja ya thamani inatokana na mitaji isiyoonekana ikiwemo chapa, ubunifu na teknolojia.

    Baada ya kutafiti takwimu kuhusu shughuli ya simu za mkononi za kisasa, ripoti hiyo imegundua kuwa teknolojia ya makampuni ya simu za mkononi ya China imeongezeka kwa kasi. Mashirika ya China ikiwemo Huawei, Xiaomi, Oppo na Vivo yameingia katika nafasi kumi za mwanzo katika uuzaji wa simu za mkononi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako