• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la kimataifa la ushirikiano wa uzalishaji wa kiviwanda kwa mwaka 2017 lafanyika ili kuhimiza ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

    (GMT+08:00) 2017-11-21 18:21:16

    Kongamano la kimataifa la ushirikiano wa uzalishaji wa kiviwanda kwa mwaka 2017 na mazungumzo ya 9 ya ushirikiano na uwekezaji wa China kwa nchi za nje yamefanyika leo hapa Beijing. Washiriki kutoka ndani na nje ya China wametoa maoni yao kuhusu jinsi ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa wa uzalishaji wa kiviwanda ili kusukuma mbele ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

    Hayo ni mazungumzo ya kwanza ya ngazi ya kimataifa kuhusu "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na "ushirikiano wa kimataifa wa uzalishaji wa kiviwanda" kufanyika baada ya mkutano mkuu wa 19 wa Chama, ambayo yamehudhuriwa na wadau wa siasa, biashara na taaluma wapatao elfu tatu kutoka nchi na sehemu 116 duniani.

    Kwenye sherehe ya ufunguzi, naibu katibu mkuu wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China Zhou Xiaofei amesema katika miaka ya hivi karibuni, China imeweka kipaumbele katika ujenzi wa "Ukanda Moja, Njia Moja", kuhimiza ushirikiano wa kimataifa wa uzalishaji wa kiviwanda, na kuunga mkono makampuni yenye uwezo kwenda nje ya China. Hivi sasa, China imesaini nyaraka kuhusu uzalishaji wa kiviwanda na ushirikiano wa uwekezaji na nchi 35, na kuanzisha utaratibu wa kufanya ushirikiano katika soko la tatu na Ufaransa, Ujerumani na Canada, na kufanya ushirikiano wa pande nyingi wa uzalishaji wa kiviwanda na Jumuiya ya Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia ASEAN, Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya.

    Bw. Zhou Xiaofei amesema ushirikiano huo umetimiza malengo ya kusaidiana na kunufaishana.

    "Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2016, wawekezaji wa China wameanzisha makampuni elfu 37 yanayowekeza katika nchi za nje, na uwekezaji huo umefikia dola za kimarekani trilioni 1.4. Mwaka 2016, kodi zilizotolewa na makampuni ya China yanayowekeza nje ya nchi zilifikia karibu dola za kimarekani bilioni 30, na kuwaajiri wafanyakazi wa kigeni milioni 1.303, idadi ambayo iliongezeka kwa watu laki 1.18 kuliko mwaka 2015."

    Wakati wa kuunga mkono makampuni ya China kwenda nchi za nje, China pia imeboresha mazingira yake ya ndani, na kujitahidi kuvutia uwekezaji kutoka nje. Bw. Zhou amesema kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Kamati ya Biashara na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, China imekuwa nchi inayopata uwekezaji kutoka nje kwa wingi zaidi. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, China imevutia uwekezaji wa zaidi ya dola za kimarekani trilioni 1.8. China inaongoza miongoni mwa nchi zinazoendelea kwa miaka 25 mfululizo katika kuvutia uwekezaji kutoka nje, na kuwa nafasi ya tatu duniani kwa miaka tisa mfululizo.

    Akizungumzia siku za baadaye, Bw. Zhou amesema ripoti ya mkutano mkuu wa 19 wa chama imesema mlango wa China utafunguliwa kwa nje, na utazidi kuwa wazi. China itahimiza kwa kiwango cha juu uhuru na urahisi wa biashara na kuvutia uwekezaji kutoka nje.

    Mshauri wa rais wa Russia anayehudhuria mazungumzo hayo Sergey Glaziev anaona kuwa kuhimiza nakuunganisha mafungamano ya uchumi kati ya Ulaya na Asia na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kutasaidia ongezeko la biashara. Amedokeza kuwa kazi husika zinafanyika taratibu.

    "Kabla ya wiki kadhaa, mafungamano ya uchumi kati ya Ulaya na Asia yakiwa upande mmoja na China ikiwa upande mwingine tumekamilisha kazi za kusaini makubaliano ya utaratibu, na ndani ya makubaliano hayo, tunaweza kujenga mazingira mazuri ya uwekezaji. Makubaliano hayo yametaja kupunguza na kuondoa vikwazo vya kiteknolojia na kulinda hakimiliki, na hivi karibuni tutaweza kusaini makubaliano hayo, hatua ambayo itakuwa muhimu kwa kuunganisha mafungamano ya uchumi kati ya Ulaya na Asia na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja"."

    Aliyekuwa waziri mkuu wa Ufaransa Jean-Pierre Rafrin amesema kwenye hotuba yake kuwa hali ya makadirio na usalama ni msingi wa maendeleo ya uchumi na uwekezaji, na ametoa wito wa kuangalia upande wa mashariki. Amesema China imetoa pendekezo la kujenga "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kuanzisha Benki ya Uwekezaji wa Miundo mbinu ya Asia AIIB na Mfuko wa njia Hariri, bidhaa hizo zinahitajika duniani.

    "Kwa nini tunapongeza hatua inayochukuliwa na serikali ya China, kwani katika mashirika ya kimataifa kama Umoja wa Mataifa na Shirika la Afya Duniani WHO, na Benki ya AIIB na Mfuko wa njia ya Hariri, mipango iliyotolewa na China yote inafuata sera ya kushirikisha pande nyingi, na dunia inahitaji sera hiyo kuhimiza amani."

    Imefahamika kuwa mbali na sherehe ya ufunguzi ambayo ni kongamano kuu, makongamano mengine 26 yatafanyika kati ya nchi tofauti, kanda tofauti na sekta tofauti. Wakati wa shughuli hizo, ripoti ya maendeleo ya sekta za China katika nchi za nje kwa mwaka 2017 itatolewa, ili kuhudumia makampuni ya China kufanya shughuli zao nje ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako