• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Watafiti Uganda kuzalisha ndizi kwa njia ya kibaiolojia yaani GMO ifikapo mwaka 2021.

    (GMT+08:00) 2017-11-21 18:43:44

    Watafiti kwenye maabara za utafiti wa kilimo cha Kawanda nchini Uganda wamesema wako tayari kuzalisha ndizi kwa njia ya kibaiolojia yaani GMO ifikapo mwaka 2021.

    Hii inafuatia kipitishwa kwa sheria ya kitaifa kuhusu usalama wa vyakula vinazyozalishwa kwa njia hiyo.

    Sheria hiyo sasa inasubiri kutiwa saini na rais baada ya kupitishwa na bunge.

    Mtafiti mkuu kwenye kituo hichp Dkt Priver Namanya Bwesigye, amesema wana teknolojia kadhaa ambazo ziko tayari kutumika kuzalisha ndizi kwa njia ya kibaiolojia.

    Bwesigye amesema watafanyia majaribio kwa mashamba ya wakulima ili kuhakikisha migomba hiyo inaweza kuhimili magonjwa na hali mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako