• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashindano ya Kriketi ya Nairobi

    (GMT+08:00) 2017-11-22 10:27:50
    Mambo yamebadilika kwenye msimamo wa ligi ya mchezo wa Cricket kwa timu za Nairobi nchini Kenya baada ya timu Swamibapa kushinda kwa mikombio 49 dhidi ya klabu ya Kanbis kwenye mechi iliyofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya EastLegh.

    Licha ya ushindi huo kuipunguza kasi Kanbis, haukuisaidia Swamibapa kwani bado inasalia katika nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kujikusanyia alama 219 nyuma ya hao Kanbis ambao wanabaki katika nafasi ya pili kwa kuwa na alama 230.

    Vinara wa ligi hiyo yenye timu kumi ni Stray Lions ambayo ina jumla ya alama 266, nafasi ya mwisho kwenye msimamo imekamatwa na Kongonis yenye alama 71 pekee.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako