• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matokeo ya mechi za ligi ya klabu bingwa Ulaya

    (GMT+08:00) 2017-11-22 10:28:25
    Klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza jana imeshindwa kulinda uongozi wa magoli matatu iliyofunga katika kipindi cha kwanza dhidi ya Sevilla kwenye mechi ya raundi ya tano ya hatua ya makundi katika ligi ya klabu bingwa Ulaya.

    Magoli hayo yaliyofungwa na Roberto Firmino mawili na Sadio Mane moja, yalidumu kipindi cha kwanza tu kabla ya Sevilla kusawazisha yote katika dakika za 51, 60 na 93 kupitia Wissam Yedder mawili na Guido Pizzaro.

    Kufuatia matokeo hao, timu hizo ambazo ziko kundi E la michuano hiyo, zitasubiri hadi mechi ya mwisho ya makundi ili kujihakikishia kufuzu hatua ya 16 bora, kwa kuwa Liverpool ni vinara kwa pointi 9, Sevilla 8 na Spartak Moscow wako nafasi ya tatu wakiwa na alama 6 ambazo endapo wakishinda mechi ya mwisho dhidi ya Liverpool wanaweza kufuzu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako