• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Besiktas yafuzu hatua ya 16 Boraklabu bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza

    (GMT+08:00) 2017-11-22 10:28:43
    Kwa mara kwanza klabu ya Besktas ya Utruruki imefuzu hatua ya 16 bora katika michuano ya klabu bingwa Ulaya licha ya kupata matokeo ya sare ya goli 1-1 na FC Porto.

    Besiktas imefikisha pointi 11 na ni vinara wa kundi G, ikiwa imeshinda mechi 3, na kutoa sare mbili, lakini FC porto na RB Leipzig watalazimika kusubiri mechi za mwisho ili kujihakikishia nafasi moja iliyosalia katika kundi hilo.

    Timu zingine zilizofuzu jana kuingia hatua ya kumi na sita bora ni Real Madrid ya Hispania na Tottenham Hotspurs ya Uingereza.

    Madrid imefuzu kwa kuwa mshindi wa pili wa kundi baada ya kuifunga Apoel Nicossia ya Cyprus kwa magoli 6-0, na Tottenham wakiibuka vinara wa kundi hilo kwa kufikisha pointi 13 baada ya kuifunga 2-1 Borussia Dortmund jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako