• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara wa Rwanda wamehimizwa kutumia bandari ya Mombasa kutokana na miundombinu mipya bandarini humo

    (GMT+08:00) 2017-11-22 19:19:27

    Jamii ya wafanyabiashara wa Rwanda wameshauriwa kutumia bandari ya Mombasa kutokana na miundombinu mipya iliyowekwa bandarini humo ili kuongeza biashara.

    Mkurugenzi Mkuu wa Halmashauri ya Bandari nchini Kenya (KPA) Bi Catherine Mturi-Wairi amesema halmashauri hiyo imejitolea kufanikisha biashara ya kikanda kwa kutoa huduma za haraka na bora,na kuongeza kuwa wanatarajia kuongeza utendaji wa bandari ya Mombasa kufikia viwango vya kimataifa.

    Alisema wanashughulikia mpango ambao utapunguza zaidi ucheleweshwaji katika bandari hiyo.

    Aidha alisema tayari wameongeza yadi na vituo vya kupakua na kupakia mizigo,kuboresha mfumo ya kompyuta kwa ajili ya uharakishaji wa stakabadhi,na kuongeza vifaa vya kisasa ili vya kushughulikia mizigo mingi zaidi.

    Bandari hiyo hivi karibuni iliwkeza zaidi ya $1 billioni kupanua vifaa vyake ili kuongeza uwezo wake wa kushughulikia mizigo mingi zaidi.

    Bandari ya Mombasa ilishughulikia jumla ya tani 22,756,448 za shehena katika kipindi cha mwezi Januari hadi Septemba ikilinganishwa na tani 20,566,156 zilizoandikishwa kipindi sawa na hicho mwaka 2016,ikiashiria ongezeko la tani 2,190,293 tau asilimia 10.6.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako