• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yaionya Kenya juu ya hatari ya madeni

    (GMT+08:00) 2017-11-22 19:20:27

    Shirika la Fedha Duniani,IMF,limeionya Kenya kwamba viwango vya madeni vya nchi hiyo vinafaa kudhibitiwa ili kuuzuia uchumi kutokana na misukosuko.

    Mwakilishi wa IMF nchini Kenya Jan Mikkelsen amesema japo uchumi umeonyesha kustahmili ukame na kipindi kirefu cha uchaguzi,madeni makubwa ya umma yanayoongezeka yanatia wasiwasi na yanafaa kuangaliwa ili kuepuka misukosuko yoyote kwa uchumi siku zijazo.

    Madeni ya umma ya Kenya yamekuwa yakiongezeka katika miaka ya hivi karibuni,na kufikia Sh4.4 trillioni mwezi Septemba kutoka chini ya shilingi trilioni moja katikati ya mwaka 2014.

    Ripoti ya Mapitio ya Bajeti (BROP) iliyotolewa mwezi Septemba imeonyesha kuwa kiwango cha madeni ya umma dhidi ya uwiano wa pato la taifa ulitarajiwa kuongezeka hadi 59% katika mwaka huu wa fedha,kutoka malengo ya awali ya 51.8%.

    Upungufu wa fedha ulionekana katika 7.9% kutoka utabiri wa awali wa 6.2%.

    Mwakilishi huyo alisema ujumbe wa IMF utazuru Nairobi katikati ya mwezi Desemba kupitia upya mipango yake na serikali ya Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako