• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-TCB yazindua rasmi msimu wa upandaji pamba

    (GMT+08:00) 2017-11-22 19:20:48

    Bodi ya pamba Tanzania (TCB) jana ilizindua rasmi msimu mpya wa kilimo cha pamba katika kanda ya magharibi kwa mwaka 2017/2018.

    Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Mkurugenzi Mkuu wa TCB ,Marco Mtunga,alisema msimu huo unahusisha mikoa ya Mwanza,Simiyu,Shinyanga,Geita,Tabora,Mara,Kagera,Singida,Kigoma na Katavi.

    Aidha Mtunga alisema katika msimu huu,tani 25,000 za mbegu zimetengwa zikijumuisha tani 11,548 za mbegu mpya ya UKM08 na tani 13,452 za mbegu ya UK91.

    Mkurugenzi huyo alisema serikali kwa kushirikiana na wadau imefufua mfumo wa kuzalisha mbegu bora za kupanda na kwamba azma ni kuwapatia wakulima mbegu bora ili kuhakikisha mafanikio makubwa yanapatikana katika kilimo hicho.

    Alisema katika msimu huu,jumla ya ekari milioni 1.3 zinatarajiwa kupandwa pamba katika msimu wa kilimo wa 2017/2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako