• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China kujenga kiwanda cha uunganishaji matrekta

    (GMT+08:00) 2017-11-22 19:21:07

    Kampuni ya Juren Group ya China inatarajia kujenga kiwanda cha uunganishaji matrekta eneo la Misugusugu mjini Kibaha ili kuinua sekta ya viwanda na kuimarisha kipato cha wananchi.

    Aidha kampuni hiyo kwa kushirikiana na Shirikisho la vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) wanatarajia kuchimba visima virefu na mabwawa ili kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya umwagiliaji.

    Viongozi wa Juren Group wameahidi kuanza kutengeza matrekta hayo nchini Tanzania badala ya kuunganisha iwapo mazingira ya uwekezaji yatakuwa mazuri.

    Ofisa Uhusiano wa mamlaka ya ukanda maalum wa uwekezaji (EPZ) ,Nyanda Shuli aliwashauri wawekezaji hao kuwa licha ya uunganishaji wa matrekta ,wajitahidi kuanza uzalishaji wa bidhaa zao nchini Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako