• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Manchester United yavutwa shati klabu bingwa Ulaya

    (GMT+08:00) 2017-11-23 14:47:26

       

    Manchester United iliyokuwa inahitaji matokeo sare kwenye mechi ya jana ili kufuzu hatua ya 16 bora kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya, sasa italazimika kusubiri hadi mechi mwisho ya hatua ya makundi baada ya jana kufungwa FC Basel ya Uswisi kwa goli 1-0.

    Katika mechi ya mwisho mwezi ujao, Manchester United yenye pointi 12, itakuwa nyumbani kuikaribisha CSKA Moscow ya Urusi yenye 9, na mchezo huo ukitazamiwa kuwa mkali, kwa kuwa timu zote zinayo nafasi ya kufuzu kwa hatua inayofuata.

    Lakini timu zilizofuzu baada ya mechi za jana ni, Chelsea iliyopata ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya FC Qarabag, Barcelona baada ya kupata sare ya 0-0 na Juventus.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako