• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuongeza kasi ya kuhimiza maendeleo ya usafirishaji bidhaa kwa vyombo vya usafiri visivyopungua viwili

    (GMT+08:00) 2017-11-23 17:40:52

    Katika miaka ya hivi karibuni, China imetumia usafirishaji wa bidhaa kwa kutumia vyombo vya usafiri visivyopungua viwili kuhimili mfumo wa uchumi wa kisasa, kuongeza kasi ya ujenzi wa mfumo wa usafirishaji wa kisasa, na kupunguza gharama na kuongeza ufanisi wa usafirishaji bidhaa. Hatua hii imepata mafanikio ya mwanzo.

    Usafirishaji wa bidhaa kwa kutumia vyombo vya usafiri visivyopungua viwili unaweza kutumia ipasavyo nguvu za reli, barabara, bahari na anga, kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za usafirishaji bidhaa.

    Kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zhengzhou, mji mkuu wa mkoa wa Henan, katikati ya China, kuna ukumbi ambao taarifa kuhusu safari za ndege za mizigo na ghala za kuhifadhia mizigo zinaonesha na kubadilika kwa wakati. Naibu meneja wa kampuni ya Henan ya usafirishaji wa mizigo kwa ndege, Xu Hongyan amesema, moja ya kazi zao ni kusafirisha mizigo kutoka uwanja wa Zhenghou hadi maeneo mbalimbali. Anasema,

    "Pia tunachukua bidhaa zitakazouzwa nje ya nchi kutoka ghala nyingine hadi kwenye ghala letu la kimataifa katika uwanja wa ndege, na kuziweka kwenye ndege. Sasa tumetimiza lengo la kufanya bidhaa kusafirishwa kutoka njia ya barabarani hadi njia ya anga bila tatizo katika kushughulikia uagizaji na uuzaji bidhaa nje."

    Hivi sasa, maeneo mbalimbali nchini China yametimiza muundo wa kusafirisha bidhaa kwa njia ya barabara, reli, bahari na anga kwa wakati mmoja. Msemaji wa Wizara ya Uchukuzi ya China Wu Chungeng amesema, Wizara hiyo inaongeza nguvu ya kuunga mkono ujenzi wa maeneo ya kuunganisha njia hizo mbalimbali za usafirshaji wa bidhaa.

    "Hivi sasa, serikali ya China inaungaji mkono kifedha maeneo ya usafirishaji bidhaa yenye huduma za kusafirisha bidhaa kutoka chombo kimoja cha usafiri hadi kingine. Mpangilio wa maeneo ya usafirishaji bidhaa kwa njia ya usafiri wa barabarani umeboreshwa, na kwamba vituo 12 vya makontena na bandari 8 za nchi kavu za reli zimejengwa. Miji zaidi ya 70 kote nchini pia inapanga kujenga maeneo yanayotoa huduma za kusafirishaji bidhaa kutoka chombo kimoja cha usafiri hadi kingine."

    Takwimu zinaonesha kuwa katika nchi zilizoendelea, usafirishaji wa bidhaa kwa makontena kupitia njia za bahari na reli unafikia asilimia 20 hadi 40, lakini China ni asilimia mbili tu; usafirishaji bidhaa kwa makontena unachukua asilimia 30 ya usafirishaji bidhaa kwa njia ya reli katika nchi zilizoendelea, lakini China ina asilimia 10 tu. Kwa sababu hiyo, China bado iko katika kipindi cha mwanzo kwa maendeleo ya usafirishaji bidhaa kwa vyombo vya usafiri visivyopungua viwili. Msemaji wa Wizara ya Usafiri ya China Wu Chungeng amesema katika siku zijazo, Wizara hiyo itaongeza ubora wa huduma za usafirishaji bidhaa kwa vyombo vya usafiri visivyopungua viwili, kupunguza gharama na kuongeza ufanisi wa usafirishaji bidhaa, na kujenga mfumo wa usafirishaji bidhaa kwa vyombo vya usafiri visivyopungua viwili wenye gharama nafuu, salama na ufanisi na usiochafua mazingira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako