• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia:Ethiopia yapata tuzo ya nchi bora ya uwekezaji 2017

    (GMT+08:00) 2017-11-23 19:33:58

    Ethipia imetuzwa kama nchi bora ya uwekezaji mwaka 2017 kwa ufanisi wake wa kuvutia wawekezaji na kuweka mazingira bora ya miradi ya maendeleo.

    Tuzo hizi za shirika la umoja wa mataifa zimetolewa katika awamu ya 9 ya kongamano la umoja wa mataifa la biashara na maendeleo nchini Uhispania.

    Ethiopia imetambuliwa na kutuzwa kutokana na juhudi za serikali na sekta binafsi na taasisi za biashara katika kufanikisha fursa za uwekezaji.

    Sekta ya leba,viwanda,utalii ,miundo msingi zimefungua fursa nyingi za uwekezaji zilizobuni ajira kwa vijana na wanawake.

    Hivi karibuni tu serikali ya Ethiopia imepewa tuzo za kutoa huduma bora za beni pamoja na kuweka sheria bora za uwekezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako