• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Mashirika binafsi yaungana na Umoja wa mataifa kukabiliana na ukosefu wa chakula

    (GMT+08:00) 2017-11-23 19:49:29

    Maafisa wa serikali katika kanda ya Afrika Mashariki na wataalamu wa Umoja wa mataifa wameungana na sekta binafsi katika kukabiliana na ukosefu wa chakula na athari zake za uchumi.

    Katika kongamnao la siku mbili la majadiliano ya chakula na lishe bora huko Kigali, maafisa hao wameangazia kupungua kwa ukuwaji wa uchumi kutokana na ukosefu wa chakula.

    Kongamano hili limehudhuriwa na wajumbe kutoka shirika la chakula duniani FAO na shirika la mpango wa chakula WFP.

    Wataalamu hao kutoka nchi za Rwanda,Kenya,Tanzania,Ethiopia na nyinginezo wamesema Ethiopia ndio nchi ya kwanza inayoyumbishwa kiuchumi kutokana na ukosefu wa chakula cha kutosha katika baadhi ya mikoa.

    Tanimoune Mohamadou mtaalamu wa masuala ya lishe bora amesema bara la Afrika linakosa kug=fikia malengo yake ya kiuchumi kutokana na changamoto za kilimo na chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako