• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Ufisadi nchini Tanzania wapungua

    (GMT+08:00) 2017-11-23 19:50:07

    Utafiti mpya wa uchumi na biashara nchini Tanzania umeonyesha, viwango vya rushwa vimepungua nchini humo kwa mwaka 2017 ikilinganishwa na miaka 10 ilyopita..

    Aidha, utafiti huo umebainisha kwamba, wananchi wameripoti kuwa uzoefu wao wa kuombwa rushwa umepungua katika sekta zote mwaka huu ikilinganishwa na 2014.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze amesema mitazamo ya utafiti huo unatokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mkononi.

    Matokeo hayo yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,705 kutoka maeneo mbalimbali Tanzania Bara kati ya Julai na Agosti mwaka huu," alibainisha Eyakuze.

    Matokeo hayo ya utafiti yanatia matumaini ikilinganishwa na miaka mitatu iliyopita, ambako wananchi wamekuwa na mtazamo chanya kuhusu mafanikio yanayojitokeza kutoka katika mapambano dhidi ya rushwa.

    Mwakilishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Sabina Seja alisema rushwa bado ipo na kuwataka wananchi na wadau mbalimbali kutoa ushirikiano katika kupambana nayo badala ya kuiachia serikali pekee.

    Naye Ludovick Utouh aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), alisema ni kweli kwa kipindi hiki rushwa imepungua tofauti na miaka ya nyuma na kuwataka Watanzania kuichukia rushwa.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze, alisema wananchi wanaripoti kuombwa rushwa katika sekta mbalimbali kumepungua ambapo kwa upande wa polisi ilikuwa asilimia 60 mwaka 2014 hadi asilimia 39 mwaka 2017, Ardhi asilimia 32 mwaka 2014 hadi asilimia 18 mwaka huu, Afya asilimia 19 mwaka 2014 hadi asilimia 11 mwaka huu.

    Hata hivyo, alisema wananchi wapo tayari kujitolea ili kupunguza rushwa ambapo asilimia 81 walikubali kuwa ni muhimu kupambana na rushwa hata kama itachelewesha maendeleo wakati asilimia 19 wanasema kusiwe na ukali kwa kuwa itaathiri uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako