• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:uharibifu wa miundo msingi waathiri technolojia ya mawasiliano

    (GMT+08:00) 2017-11-23 19:50:27

    Mkurugenzi mkuu wa halmashauri ya mawasiliano hapa nchini CA Francis wangusi ameibua wasi wasi kutokana na ongezeko la hivi majuzi la visa vya uharibifu wa muundo msingi wa teknolojia ya habari na mawasiliano katika baadhi ya sehemu za nchi hii.

    Wangusi amesema visa hivyo vimesababishwa na mashambulizi ya magaidi hasa katika kaunti za Mandera, Garissa na baadhi ya sehemu za kaunti ya Lamu, huku uharibifu wa vikingi vya mawasiliano ya simu na moundo msingi mingine ukishuhudiwa pia katika baadhi ya sehemu za nchi hasa katika kaunti ya Kisumu baada ya kipindi cha uchaguzi kilichokamilika hivi punde.

    Amesema uharibifu wa muundo msingi wa teknolojia ya ICT umesababisha hali ya kukatika kwa mtandao na huduma katika maeneo yaliyoathirika na kuhatarisha maisha ya wakenya .

    Wangusi vile vile amesema visa vya wahalifu na magaidi kuharibu muundo msingi huo vimeathiri vibaya sekta ya ICT na huduma nyingine muhimu kama vile huduma za benki na fedha , usalama wa kitaifa na biashara. Hata hivyo amesema serikali tayari imetayarisha mswada unaolenga kushinikiza serikali kuupa muundo msingi wa mawasiliano hapa nchini ulinzi wa kutosha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako