• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda ndio Vinara wa Afrika Mashariki

    (GMT+08:00) 2017-11-24 09:37:45
    Uganda (The Cranes) imeendelea kuwa vinara katika viwango vya soka katika ukanda wa Afrika Mashariki ikiwa ni kwa mujibu wa viwango vya soka duniani kwa mwezi novemba.

    Lakini licha ya kuongoza, Uganda pia imeshuka kwa nafasi 4, hadi 74 kidunia kufuatia matokeo yake kwenye mechi za kimataifa ilizoshiriki mwezi novemba.

    Kenya ni ya pili kwa Afrika Mashariki ikiwa ya 111 duniani, Rwanda nafasi ya tatu Afrika mashariki na 120 duniani, Burundi, Tanzania na Sudan Kusini zinakamata nafasi ya nne tano na sita mtawalia.

    Kimataifa, Ujerumani imeendelea kuongoza kwenye msimamo kwa kuwa na alama 1602 ikifuwatiwa na Brazil yenye 1483.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako