Uamuzi huo waweza kuchukuliwa endapo serikali itapitisha muswada uliopelekwa bungeni wa kuitaka serikali iingilie masuala ya soka nchini humo.
FIFA sasa watalazimika kutafuta timu mbadala iwapo Peru watafutwa.
Lakini gazeti la Libero la nchini Peru limemnuku mbunge ambaye amahusika kupeleka muswada huo Paloma Noceda akiwatoa wasiwasi wananchi wa Peru kuwa hata sheria ipitishwe timu itashiriki kombe la dunia.
Peru hawajashiriki kombe la dunia tangu mwaka 1982, na awamu hii wamefuzu baada ya kuwafunga New Zealand kwenye mechi ya mtoano.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |