• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi ya Yuropa, Arsenal na Everton zafungwa

    (GMT+08:00) 2017-11-24 10:19:54

    Licha ya kusalia kuwa vinara wa kundi H, na ikiwa imefanikiwa kufuzu kwa hatua ya 16 bora ya michuano ya ligi ya Yuropa, klabu ya Arsenal jana imekubali kipigo cha goli 1-0 ikiwa ugenini nchini Ujerumani ilipocheza na FC Cologne.

    Goli la FC Cologne limefungwa kwa njia ya penati mnano dakika ya 62 baada ya Mathieu Debuchy kucheza rafu katika eneo la hatari.

    Nayo timu nyingine ya Uingereza, Everton imeendeleza rekodi mbaya ya kufungwa katika michuano hiyo, baada ya kukubali kipigo kikubwa cha magoli 5-1 ikiwa nyumbani dhidi ya Atalanta ya Italia ikiwa ni kipigo cha nne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako