• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa kanda ya Afrika mashariki unatarajiwa kukua zaidi mwaka ujao

    (GMT+08:00) 2017-11-24 19:21:48
    Uchumi wa kanda ya Afrika mashariki unatarajiwa kukua mwaka ujao hasa katika sekta za mawasiliano, uchukuzi na ujezi.

    Uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua kwa asilimia 7.1 ikilinganishwa na asilimia 7 ya mwaka huu.

    Waziri wa fedha nchini humo Philip Mpango ameahidi kuongeza uwekezaji wa serikali kwenye sekta za miundo mbinu kama vile ujenzi wa reli mpya ya kisasa, barabara na bandari.

    Serikali nchini humo inatarajia kukopa dola milioi 600

    Wiki iliopita katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Liberat Mfumukeko alipokea dola miloni 1.5 kutoka kwa benki ya maendeleo ya Afrika za ujenzi wa barabara kati ya Masaka nchini Uganda na Kumunazi nchini Tanzania.

    Nchini Kenya waziri wa fedha anasema kilimo mwaka ujao ndio kitasaidia ukuaji mkubwa wa uchumi.

    Na nchini Uganda uchumi unatarajiwa kukua kwa asilimia 5 nao ule wa Rwanda ukikua kwa kati ya asilimia 6 na 7.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako