• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo walalamikia gharama za uondoshaji mzigo

    (GMT+08:00) 2017-11-24 19:23:19
    Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo mjini Dar es salaam nchini Tanzania wamelalamikia gharama za uondoshaji mzigo bandarini kudumaza ufanisi wa shughuli zao.

    Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo (JWK), Abdallah Mwinyi amesema soko hilo liko mbioni kupotea endapo jitihada za kulinusuru hazitafanyika.

    Alisema hilo linatokana na changamoto wanazokutana nazo Bandari ya Dar es Salaam ambako kuna mlolongo mrefu wa kukamilisha taratibu za kuondosha mzigo unaoingizwa na kuwapo kwa makadirio makubwa ya tozo zinazotakiwa kulipwa jambo linalowakatisha tamaa.

    Mwinyi alisema mzigo wa aina moja unaoingizwa na watu wawili tofauti bandarini hapo hutozwa kiasi kisicholingana. Wapo wanaopata unafuu wakati wengine wanaumia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako