• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Juhudi za kupambana na maambukizi ya Ukimwi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

  (GMT+08:00) 2017-11-27 13:41:44

  Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, viongozi wa serikali mitaani wamefanya juhudi kubwa katika kupambana na maambukizi ya Ukimwi.

  Nao madaktari wanakataa ubaguzi dhidi ya wagonjwa wa Ukimwi wakitoa tahadhari kwa watu wanaowabagua, huku wakionyesha hatua zilizochukuliwa na serikali kuhusu watu wanaoishi na virusi vya HIV.

  Viongozi hao walianza kuwahimiza kwa ajili ya kuokoa ndoa nyingi zinazoweza kuangamia endapo kutakuwa tofauti zitakazowatenganisha kwa muda.

  Mume na mke watakapovunja unyumba wao kwa muda wa mwezi moja miwili, au zaidi na kupenda kurudishana tena, wametakiwa kabla ya kukutana kimwili, kwenda kwenye kituo cha afya ili kila mmoja afahamu hali ya mwili wake, kuona katika kipindi hicho cha matengano, hakuna aliyekwenda kando na kupatwa na virusi vya HIV asije akaambukize mwenzie.

  Bwana EUPHREM KANDONDO ni mwenyekiti wa Baraza la Usalama mjini MANGINA kilomita thelathini Magharibi mwa Kinshasa, akizungumzia madhumuni ya kampeni hiyo alisema, wameanza kuwatuka kule ili kila mmoja kati ya mume na mke, hakuna mtu aliyekwenda nje ya ndoa, asije akaambukize mwenzake.

  Ili kueneza ujumbe kwa taabaka mbalimbali. Viongozi wa miji, walianza vikao vya kuwahimiza hata wale viongozi wa msingi. Wataalamu walitoa njia mbalimbali za maambukizi pamoja na zile ambazo zinaweza kusaidia kama vile kinga, kusudi mtu asiambukizwe, wakigusia kanuni tatu muhimu, moja ikiwa ni kujizuiza kutenda kitendo cha ngono nje ya ndoa, pili ni kuwa muaminifu, na tatu ikiwa ni kutumia mpira wa kinga au Condom kama walivyodokeza.

  Amesema viongozi wanaendelea kuwahimiza watu tukiwaambia kwamba kuna kanuni tatu ambazo zinaweza kuwasaidia kuepukana na magonjwa ya Ukimwi ukitumia, au kujizuiza, kuwa mwaminifu kati ya mume na mke, na kwa mwisho kutumia mpira ya kinga yaani Condom kwa kuwa watu wanaendelea kuzunguka na mipira ya kinga huku na huku.

  La sivyo cha muhnimu ni kuenda kujipima ili ufahamu hali yako.

  Mwanamka mmoja miongoni mwa wale wanatoa onyo kwa wahanga wa magonjwa ya Ukimwi, ametoa mwito kwa wahusika, kuwa na juhudi ya kujitetea kwamba ni mgonjwa, bila ya kuwa na aibu kwa ajili ya kuwaokoa watu wengi na kusema.

  Watu wanapojitambua kuwa wagonjwa wa Ukimwi, lazima wafahamu kwamba Ukimwi ni ugonjwa kama mwingine, na hakuna haja ya kuwa na aibu. Bila shaka watu wanaoishi na virusi vya HIV, wana haki ya kuishi kama binadamu wengine, mfano wanaoambukizwa malaria, mafua, homa na kadhalika.

  Daktari JUSLAIN MAYAO ambaye ni mtaalamu wa uvumbuzi wa dalili za magonjwa amesema swali hilo ni la muhimu katika jamii kwa siku hizi hasa barani Afrika. Hofu inawatia watu kwa sababu hadi kufikia leo ugonjwa huo ahujapata tiba kamilifu, na endapo mtu atajitambua kuwa tayari ameambukizwa, anachokiona mbele yake ni kifo. Vilevile kuna aibu ambayo watu wengi wanafikiria endapo watakutwa na virusi vya HIV, kila mtu atafikiria aliyapata kupitia njia ya ngono.

  Na tatu ni kwamba, mara mtu anapojitambua au anapojuliwa kwamba amepatwa Ukimwi, mara na mara watu hao wabaguliwe katika jamii, jambo ambalo linapigwa marufuku na serkali kwa kuwa wagonjwa hao ambao wana haki ya kuishi kama watu wengine.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako