• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafungua soko la huduma kwa wazee

    (GMT+08:00) 2017-11-27 17:30:16

    Naibu katibu mkuu wa kamati kuu ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Shi Zihai leo hapa Beijing amesema, hadi kufikia mwaka 2016, idadi ya wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60 nchini China ilikuwa zaidi milioni 230, na inakadiriwa kufikia milioni 480 hadi kufikia katikati ya karne hii. Amesema katika siku zijazo, China itaharakisha kuendeleza huduma kwa wazee, na kufungua soko la huduma hizo kwa nchi nyingine duniani.

    Kongamano la kimataifa kuhusu maendeleo ya huduma kwa wazee limefanyika leo hapa Beijing. Naibu katibu mkuu wa kamati kuu ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Shi Zihai ametoa hotuba akisema, katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na ongezeko la mfululizo la wazee, China inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maendeleo ya kutosha na uwiano wa huduma kwa wazee. Anasema,

    "Mwaka jana, idadi ya wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60 nchini China ilizidi milioni 230, na kuchukua asilimia 16.7 ya wachina wote. Idadi hiyo inakadiriwa kuongezeka na kuwa watu milioni 480 hadi kufikia katikati ya karne hii. China inatakiwa kuboresha mazingira ya kutunza wazee nyumbani, na kukamilisha mfumo wa kiserikali na kijamii wa huduma kwa wazee, kwani wawekezaji bado wana wasiwasi kuhusu uwekezaji katika huduma hizo."

    Bw. Shi Zihai amesema, hivi sasa China imetoa sera ya kuhimiza maendeleo ya huduma kwa wazee na kufungua soko la huduma hizo, na pia inaharakisha mfumo unaounganisha matunzo ya nyumbani, huduma za kijamii na huduma za kibiashara.

    Kwenye kongamano hilo, baadhi ya wasomi wamependekeza kueneza kwa pande zote majaribio ya mfumo wa bima ya huduma za muda mrefu, na kutumia vya kutosha desturi ya kuwatunza wazee nyumbani. Naibu mkurugenzi wa kamati ya kazi za wazee ya China Bw. Wu Yushao amesema kuwatunza wazee nyumbani ni njia mwafaka, nafuu na yenye ufanisi mkubwa zaidi nchini China, baadaye China inapaswa kukamilisha njia hiyo. Anasema,

    "Kuwatunza wazee nyumbani kunakabiliwa na changamoto za upungufu wa sera na huduma kutoka serikali. Wazee wanahitaji huduma bora zaidi wakati wanapotunzwa nyumbani. Hali hii inatokana na huduma dhaifu za jamii."

    Bw. Shi Zihai amedokeza kuwa tangu mwaka 2011, China imetenga zaidi ya yuan bilioni 20 sawa na dola za kimarekani zaidi ya bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa mfumo wa huduma kwa wazee. Mbali na hayo, China imeendeleza huduma hizo kwa kutoa dhamana, kuanzisha mfuko maalumu, kukopa fedha kutoka Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Asia, na kuunga mkono mashirika kuwekeza huduma hizo. Aidha amesisitiza kuwa China inafungua soko la huduma kwa wazee kwa dunia nzima.

    Mkuu wa Shirika la Uwekezaji wa Mfuko wa matunzo ya Wazee la Canada Bw. Mark Machin amesema, ana imani kubwa kuhusu uchumi wa China na maendeleo ya soko la uwekezaji nchini humo, na kuamini uwekezaji nchini China utakuwa na faida kubwa. Amesema shirika lake linafuatilia nafasi ya uwekezaji nchini China katika sekta za matunzo ya wazee, mtandao wa Internet, biashara kwa njia ya Internet, uchukuzi wa bidhaa, elimu na huduma za mambo ya fedha. Anasema

    "Uwekezaji wetu nchini China unachukua asilimia 4 ya uwekezaji wetu kote duniani, huku uwekezaji wetu nchini Marekani ukichukua asilimia 40. China inashika nafasi ya pili kwa ukubwa wa uchumi, hivyo uwekezaji wetu nchini humo utaongezeka kwa kiasi kikubwa. Naamini kuwa hadi kufikia mwaka 2030, utafikia dola za kimarekani bilioni 118 kutoka bilioni 13.4 za hivi sasa."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako