• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Serikali ya Rwanda kuongezea kuku milioni 4 mwaka 2023.

    (GMT+08:00) 2017-11-27 18:15:53

    Serikali ya Rwanda inapanga kuongezea kuku milioni 4 nchini humo ifikapo mwaka 2023.

    Waziri wa kilimo na mifugo Gerardine Mukeshimana amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza uzalishaji wa mayai kwa asilimia 143.

    Mukeshimana amesema serikali imechukua hatua hiyo ili kuboresha sekta ya ufugaji na baadaye kuimarisha viwango vya protini nchini humo.

    Taakwimu kutoka kwa wizara hiyo zinaonyesha kwamba mwaka 2010 Rwanda ilikuwa na kuku milioni 3.5 huku uzalishaji wa mayai ukiwa ni milioni 10.

    Taakwimu hizo ni ishara kwamba kwa wastani kila mtu nchini humo alikula mayai 7 kwa mwaka lakini mwaka 2016 kiwango hicho kiliongezeka hadi mayai 13 mwaka 2016.

    Aidha kilimo cha kuku nchini humo kimesaidia kuongeza uzalishaji wa nyama kutoka tani 86, 000 mwaka 2015 hadi 116,000 mwaka 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako