Kampuni hiyo, M/s Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka jijini Jiangxi, inatarajiwa kutumia miezi 36 kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 108 pamoja na miundombinu mingine.
Kwa mujibu wa taarifa ya AfDB kuhusu zabuni hiyo iliyoombwa na washiriki sita wengi wakitoka China, mradi huo utatumia Sh158.8 bilioni.
Miundombinu mingine itakayoambatana na barabara hiyo ni mitaro ya maji, madaraja na njia za mchepuko.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |